
Baada ya kukamilisha jukumu la kuwa sehemu ya Benchi la Ufundi la Simba SC na kutwaa Ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara nne Mfululizo, Kocha Msaidizi Seleman Matola ameamua kurudi shule.
Matola amerudi shule kufuatia kushiriki kwenye kozi ya ukocha ya Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF diploma B inayoendelea mkoani Morogoro, chini ya ukufunzi wa Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Oscar Milambo.
Maamuzi ya kocha huyo mzawa ambaye awali alikuwa na leseni ya ukocha ya Caf diploma C, yanamfanya kuendana na matakwa Shirikisho la soka barani Africa CAF katika michuano ya klabu bingwa barani Africa CAF kwa msimu ujao.
Msimu ujao katika michuano ya klabu bingwa barani Africa, CAF ilitoa muongozo kuwa kuanzia msimu ujao kocha msidizi msaidizi mwenye leseni ya Diploma C hataruhusiwa kukaa kwenye benchi la ufundi la klabu itakayoshiriki katika michuano ya klabu bingwa, kocha atakayeruhusiwa ni yule ambaye ana leseni ya CAF diploma B na kuendelea.
Post a Comment