} });
 


Shirikisho la soka Ugandas FUFA limetangaza Milutin ‘Micho’ Sredojevic kuwa kocha mpya wa timu ya taifa kwa mkataba wa miaka miatatu (3) akichukua nafasi ya iliyoachwa na kocha Johnathan McKinstry.

FUFA imemtangaza mkufunzi huyo raia wa Serbia kuwa kocha mpya na akiwa anarejea kukinoa kikosi hicho kwa mara ya pili baada ya hapo awali kukinoa kikosi hicho kati ya mwaka 2013 hadi 2017 na alikiwezesha kikosi hicho kufuzu fainali za AFCON mwaka 2017 ambapo ilikuwa ni kwa mara ya kwanza wanashiriki tangu mwaka 1978.

Kibarua kinacho mkabili Micho mbele yake ni kuhakikisha Uganda inafuzu kucheza fainali za kombe la Dunia na katika michezo ya kuwania nafasi hiyo Uganda imepangwa kundi E sambamba na majirani zao Kenya, Rwanda, na timu ya taifa ya Mali. Taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka la nchi hiyo imeweka wazi kuwa mkataba wa kazi wa kocha huyo utaanza rasmi Agosti 1 na Agost 3 ataongea na wanahabari.

Micho anatajwa kuwa ni miongoni mwa makocha wanaolijua vizuri soka la Afrika mpaka sasa ameshafundisha katika mataifa takliban 8 barani Afeika ikiwemo Tanzania ambapo alikinoa kikosi cha Yanga mwaka 2007. Na ameshafundisha timu kadhaa kama Timu ya taifa ya Zambia Rwanda, na vilabu ni Orlando Pirates ya Afrika kusini, Al Hilal ya Sudan, Saint George S.C. ya Etiopia na Zamalek ya Misri.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top