} });
 


Msemaji Mkuu wa Serikali, na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, Ndugu Gerson Msigwa akihojiwa amefunguka sheria zilizowekwa kwenye uchapishaji wa Magazeti.

“Sheria haituambii tufungie magazeti inasema inaweza kutowapa leseni au kufuta leseni. Sasa hivi hatufungii chombo cha habari kinapewa leseni ya kufanya kazi natumaini vyombo vya habari havitavunja sheria kwa sababu hizi sheria zimewashirikisha wadau wa habari. Atakayevunja sharia hatapewa leseni”- Gerson

“Kuhusu magazeti kufunguliwa Mh. Rais Samia Suluhu Hassan ameshatoa maelekezo wale ambao wamemaliza adhabu zao wapewe leseni waendelee na kazi zao na mchakato unaendelea” Msemaji Mkuu wa Serikali”- Gerson Msigwa

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top