} });
 

 

Baadhi ya wanafamilia ya Rais wa zamani wa Zambia, Dkt. Kenneth Kaunda wamekwenda kortini kujaribu kuzuia mazishi yake katika uwanja wa kitaifa wa Embassy Park katika mji mkuu Lusaka.

 

Kaunda alikuwa rais wa kwanza wa nchi hiyo ambaye tangu mwaka 1964 hadi 1991. Aliaga dunia mnamo Juni 17, mwaka huu akiwa na umri wa miaka 97.


Serikali baadaye iliamuru kwamba atazikwa katika eneo la Embassy Park ambapo marais wengine wa zamani wamelazwa. Mazishi hayo yanapaswa kufanyika leo Jumatano.

 

Lakini sasa baadhi ya watoto, wajukuu na vitukuu wa Kaunda wanaomba korti iruhusu kiongozi huyo wa zamani kuzikwa mahali pengine, karibu na mkewe Mama Betty Mutinkhe Kaunda.


Wanasema hii itakuwa kulingana na matakwa yake ya mwisho. Haijulikani ni wangapi katika familia ya Kaunda wanaounga mkono msimamo huu na ikiwa mazishi yataahirishwa sasa. Serikali ya Zambia haijatoa tamko juu ya suala hilo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top