} });
 


Nay wa Mitego amesema amejifunza mambo mengi hivyo hataki kuyaonyesha maisha yake kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa mwanzo akifanya ‘show off’ za mali zake kama gari, nyumba au hata mpenzi wake.

 

Msanii huyo amesema hivyo kwa sababu anaamini mashabiki wake wengi ni wale wa hali ya chini na wa mtaani hivyo hataki kuwaumiza roho kwani bado anahitaji sapoti yao kwenye shughuli zake za kimuziki.

 

“Sitaki kujionyesha tena watu wanajua kama nafanya muziki sipendi ku-show off, watu wanaonisapoti kula yao ni shida lakini wananipenda, mashabiki wangu wengi asilimia kubwa ni walala hoi, watafutaji, wamachinga wanamaisha ya kuungaunga sitaki kuwaumiza roho bado nahitaji sapoti yao,” ameeleza Nay wa Mitego.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top