} });
 

 

Ndege ya Urusi iliyowabeba Watu 28 imepoteza mawasiliano leo na kuangukia Baharini umbali wa KM 15 hadi 25 kutoka Airport na taarifa zinadai Watu wote 28 waliokuwa kwenye ndege hiyo wamefariki Dunia.

Ndege hiyo aina ya An-26 ilikuwa ikisafiri kutoka Mji Mkuu wa Rasi ya Kamchatka Petropavlovsk kuelekea Mji wa Bandarini Palana, wakati ilipotoweka na haikutua katika muda uliotarajiwa.

Ndege hiyo ilikuwa na jumla ya Abiria 22 wakiwemo Watoto wadogo na Wahudumu sita.

Itakumbukwa jana ilitolewa taarifa kuwa idadi ya waliofariki kwenye ajali nyingine ya ndege ya kijeshi ya Ufilipino aina ya C-130 imeongezeka na kufikia 50.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top