} });
 


Mara nyingi sana imekuwa ngumu kwa waimbaji/wasanii/mastaa kufunguka baadhi ya mambo ambayo wanakutana nayo katika shughuli wanazozifanya. Lakini leo muimbaji wa muziki wa Injili nchini Tanzania Paul Clement amefunguka changamoto aliyokutana nayo alipoenda studio. Kupitia ukurasa wake wa Facebook unaoitea Paul Clement ameandika haya.
"Nakumbuka mwaka 2012 siku moja nilipelekwa studio fulani na rafiki yangu ambaye aliamini nina uwezo wa kuimba vizuri sitaitaja ni studio gani. Na nilipopelekwa kwenye hiyo studio huyo producer akaniambia imba nikusikie basi nikaimba akanisikiliza.
Nilipomaliza kuimba akaniambia wewe hujui kuimba na akaongea maneno mengi ambayo yaliniumiza na akanilinganisha na waimbaji fulani ambao sitawataja akaniambia siwezi kuwafikia hao kwa uimbaji wangu. Nilijisikia vibaya basi nikaondoka kwa huzuni na machozi.
Lakini lile jambo halikunifanya nikate tamaa japo liliniumiza niliendelea mbele na kufanya kile ambacho ninakiamini. Na kwa kufupisha stori MUNGU alinifanikisha kwa viwango vikubwa sanaa na yale maneno ya yule mtu hayakutimia katika maisha yangu. Na cha kushangaza yule producer aliyeniambia maneno mabaya na mabovu siku moja nilimkuta anafunga taa kwenye event yangu tena mimi sikumuona yeye ndo aliniita ili kunisalimia na tukasalimiana vizuri wala sikumuwekeea kinyongo ndani yangu.
Napenda sana haya maneno ya my brother @joelnanauka_ yamekuwa ni maneno yangu nayoishj nayo, Alisema hivi siku moja nikiwa namsikiliza “watu mia wakisema hauwezi lakini moyon mwako ukasema unaweza basi utaweza tu, Na watu mia wakisema unaweza alafu moyoni mwako ukasema huwezi hutakaa huweze” kwa nini? Ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo, sio watu wengine wakuonavyo ndivyo ulinyo. Mtu akikuambia huwezi wewe amini kuwa unaweza maana kitakachotimia sio kile alichokisema mtu mwingine ila kile ulichokiamini na unacho kikiri.
Na cha mwisho usimdharau mtu yeyote. Waswahili wanasema usimdharau usiyemjua lakini mimi nakuambia hivi hata yule unayemjua usimdharau sababu kesho yake hupangi wewe anapanga MUNGU. Barikiwa"
Watch ULINAMAKA on my YouTube channel link on my bio
#ULINAMAKA
#ULINAMAKA
#IMAGODEI
#IMAGODEI

PAUL CLEMENT - ULINAMAKA (OFFICIAL LIVE RECORDING VIDEO)

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top