} });
 


“Kwa miaka minne ambayo nimekuwa Simba SC tayari nimeshatoa zaidi ya Tsh bilioni 21.3, kila mwaka ninatoa zaidi ya Tsh bil 5.3, kwa ajili ya usajili wa wachezaji, Makocha na hamasa. Na sasa hivi CEO (Barbara) anasema zinatakiwa za usajili, nazo napaswa kulipa mimi.” – Mo Dewji.

“Kama mpaka sasa nimeshatumia zaidi ya Tsh bil 21.3 na usajili mwingine mkubwa tutafanya, gharama za pre-season kwa hesabu yangu ya haraka zitafika Tsh bilioni 24. Leo nikisema nimetimiza zile Bilioni 20 za hisa zangu asilimia 49 si hatudaiani?” – Mo Dewji.

“Hisa zangu za asilimia 49 ni Tsh bil 19.6, kulingana na FCC wamekubali, mwanzoni tulianza na Tsh bil 21 kwa asilimia 51, ikaja Tsbil 20 kwa asilimia 50, ikafika Tsh bil 19.6 kwa 49%, nikisema nitoe Tsh bil 19.6 wachambuzi wataanza tena kwa nini hajatoa Tsh bil 20.” – Mo Dewji.

“Leo ninatoa rasmi hiyo Tsh bil 20 ili hizi kelele ziishe, hii biashara tuachane nayo, nitatoa check hapa ili tumalize. Sinunui hisa ya Simba kwa Tsh bil 19.6, ninanunua kwa zaidi ya Tsh bil 43, thamani ya Klabu imepanda kutokana na uwekezaji, hili tunapaswa kukubali.” -Mo Dewji.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top