} });
 

 

Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo amesema serikali imedhamiria kupunguza au kumaliza kabisa vifo vinavyotokana na uzazi baada ya kuwekeza kwenye ujenzi wa vituo vya afya katika kila Kata kwa ajili ya kusogeza huduma ya afya kwa wananchi.

 

Shigongo amesema hayo alipokuwa akizungumuza na wananchi wa Kata ya Nyanzenda Jimbo la Buchosa kwenye mkutano wa hadhara sambamba na kusikiliza kero za wananchi.

 

Amesema Serikali ya awamu ya sita imetoa zaidi ya Sh 750 milioni kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya viwili vya Kata ya Maisome na Kata ya Nyanzenda ambapo vikikamilika Jimbo la Buchosa litakuwa na Vituo vya afya vipatavyo 7 na Hospitali moja ya Jimbo hilo.


Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Buchosa, Maria Kapinga amesema kwa sasa kuna vituo vya afya 5 vinavyohudumia wananchi, hospitali moja ya Halmashauri pamoja na zahanati zipatazo 27.

 

Mmoja wananchi wa kata ya Nyanzenda, Anamalia Samson amesema akina na mama wajawazito na watoto wachanga walikuwa wakipoteza maisha. Kwa kukosa huduma, hivyo Kituo hicho kitakapo kamilika tatizo hilo litapungua.

 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buchosa Idama Kibanzi ambaye pia ni Diwani wa kata ya Nyanzenda amesema kutokana na ukubwa wa kata hiyo Kituo cha afya kitawasaidia Wananchi wa kata hiyo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top