} });
 

Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za Global Group zilizopo Sinza, Mori Dar es Salaam Julai 17, 2021.

MBUNGE wa Buchosa, Eric Shigongo, amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan amuondolee Mkurugenzi wa Halmashauri ya BuchosaCrispin Luanda kwani ameshindwa kusimamia mapato ya ndani.

 

Shigongo amesema hayo Julai 17, 2021 kwenye mkutano wa waandishi wa habari alipokuwa akieleza mazuri yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika ofisi za Global Group zilizopo Sinza, Mori, Dar es Salaam.


Alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) alifanya ukaguzi katika Halmashauri ya Buchosa akaja na ripoti inayoonesha ndani ya miezi mitatu ya mwaka uliopita, makusanyo ya mapato ya ndani yalikuwa shilingi milioni 108 lakini hazijapelekwa benki.


“Nianze kwa kuelezea Serikali ya Awamu ya Sita, imekuwa ikijikita sana kwenye kupeleka fedha za maendeleo kwa wananchi. Mimi ni shahidi kama Mbunge wa Buchosa, nimeshuhudia fedha nyingi zikija kwa ajili ya maendeleo,”


“Mimi mwenyewe kwenye jimbo langu nimepokea milioni 500 kwa ajili ya barabara kutoka Tarura, hii wote mnaifahamu ni juzi tu. Lakini hivi juzi tena nimepokea shilingi Bilioni 1 kwa ajili ya barabara za vijijini,”


“Kuna fedha za maji, kuna Bilioni 2.7 ya maji ambayo Ruwasa wanajenga miradi mikubwa ya maji jimboni kwangu, mradi wa Bugoro na mradi wa Kazunzu,”


“Lakini nitapokea hivi karibuni milioni 600 ambazo nimeshaahidiwa, nimeshapigiwa simu kwa ajili ya ujenzi wa sekondari moja, kila jimbo linajengwa sekondari moja na mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan,”


“Nimepigiwa simu juzi na mheshimiwa Waziri wa Tamisemi dada yangu Ummy (Mwalimu) ameniambia Eric umeangalia kwenye akaunti yako ya Zahati ya Kisaba huko Maisome, nikasema bado. Nikampigia DMO aangalie, kuna milioni 500 za ujenzi wa kituo cha Afya cha Makisio cha Maisome,”

 

“Tukiwa pale nikamueleza mheshimiwa rais ya kwamba kuna mama alikuwa amefariki kwenye wiki hiyo hiyo, akitolewa kisiwani kupelekwa kituo cha Afya cha Mwangike kwenda kujifungua kwa sababu alikuwa ametanguliza mkono… yule mama alifia kwenye mtumbwi. Mheshimiwa rais aliguswa sana na moyo wake, hizi pesa zikatumwa za kituo cha Afya cha Maisome ambako yule mama alikuwa anatokea,”

 

“Mimi nilikuwa sijawahi kuhitilafiana na Mkurugenzi wangu hata mara moja mpaka nilipoanza kufuatilia mapato ya ndani, mimi naomba mheshimiwa Rais aniondolee mkurugenzi, aniondolee idara ya uhasibu isipokuwa amuache DT (mwekahazi wa halmashauri) peke yake,”


“Mimi nilikuwa sijawahi kuhitilafiana na Mkurugenzi wangu hata mara moja mpaka nilipoanza kufuatilia mapato ya ndani, mimi naomba mheshimiwa Rais aniondolee mkurugenzi, aniondolee idara ya uhasibu isipokuwa amuache mwekahazi peke yake,” alisema Shigongo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top