} });
 


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa yote nchini kuhakikisha siri za Serikali hazisambai hovyo kwenye mitandao ya Kijamii kutokana na baadhi ya barua za Serikali kukutwa kwenye mitandao ya kijamii.

Majaliwa amesema hayo Jijini Dodoma katika mafunzo ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa na kuwaambia viongozi hao kuwa wanaowajibu wakulinda siri za Serikali hivyo kuwataka kusimamia na kudhibiti utunzaji wa siri za Serikali katika maeneo wanayofanyia kazI.

Waziri Mkuu amesema kumekuwepo na tabia kwa barua za Serikali kuonekana kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp, Instagram, twitter jambo hili ni aibu na sio usiri wa nyaraka za Serikali, hakikisheni mnalinda na kudhibiti utandawazi uliopo katika suala la utunzaji wa siri za Serikali.

Pia Majaliwa amewataka viongozi hao kuhakikisha wanasimamia watumishi wa umma hasa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili waweze kutunza siri za ofisi na kuwaelekeza kutumia mfumo unaokubalika katika utoaji wa taarifa na usambazaji wa nyaraka za serikali.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top