} });
 

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Safia Jongo amesema fisi amevamia makazi ya Watu na kumnyakua Mtoto wa mwaka mmoja na nusu kisha kukimbia nae na kumjeruhia hadi kumsababishia kifo chake.

RPC Safia amesema Wananchi watatu wamejeruhiwa pia wakati wakijaribu kupambana na fisi huyo na Mwananchi mmoja hali yake ni mbaya amelazwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Kitete.

“Askari walipofika eneo la tukio fisi alijaribu kuwashambulia pia wakafanikiwa kumuua, naomba niwatanie Watani zangu Wanyamwezi, risasi 49 zimepotea kumuua fisi, sasa huyu ni fisi wa kawaida au fisi wa Kinyamwezi!?” - RPC Jongo

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top