} });
 

 

MALCOM Ally Masoud Kipanya ni mtoto wa mtangazaji maarufu na mchora katuni, Masoud Kipanya na Sara Chande amefariki dunia leo Jumatano, Julai 28, 2021, familia imethibitisha.

 

Malcom amekuwa kitandani kwa miaka 14 akisumbuliwa na tatizo la udhaifu wa misuli unaosababisha kushindwa kufanya kitu chochote katika maisha yake.Pamoja na kukosa nafasi ya kucheza, kwenda shule, kuhudhuria birthdays na graduations za rafiki zake lakini daima aliishi kwa matumaini na furaha kuwa kesho itakuwa siku bora, Malcolm alikuwa kijana mwenye mtazamo chanya katika maisha yake na fikra zake, kwani amekuwa akiamini kuwa kuacha kulalamika ndiyo mwanzo wa kuwa na furaha maishani.

 

Akiwa hajiwezi kitandani, bado alikuwa na ndoto ambazo anataka kuzitimiza katika maisha yake, ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wagonjwa wenzake na watu wenye ulemavu na kufungua taasisi ambayo itakuwa na msaada kwa wahitaji.

Pumzika kwa amani Malcom.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top