} });
 

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Mazrui amethibitisha kuchanjwa na chanjo aina ya SINOVAC ambayo ni msaada kutokea China na kipaumbele cha chanjo hiyo itakuwa ni Wizara ya Afya, Wafanyakazi wa Airport pamoja na wanaojishughulisha na shughuli za Kitalii.

Nimechanja hapa Dawa ya SINOVAC  kutoka China tutaanza kuwachanja wafanyakazi wote wa wizara ya Afya ambao wapo mstari wa mbele kabisa kama mimi nilivyofanya na tumepata msaada kutoka Serikali ya China doze Elfu 10 kwa kuchanja watu Elfu 5 ndio ambayo tunaanza nayo kuwachanja wafanyakazi, madaktari, Manesi’- Waziri wa Afya

Kazi ya kuchanja itaendelea tutachanja watu wote wanaofanya kazi za utalii katika mahoteli na wanaotembeza wageni vilevile tutachanja wananchi wote wenye maradhi ya kisukari, Pressure lakini vilevile tutaanza wenye umri mkubwa’-Waziri wa Afya

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top