} });
 


Wanachama 17 wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) mkoani Mbeya wanashikiliwa na polisi wakituhumiwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh 188 milioni.

 

Wanadaiwa kuchukua dawa nyingi kwenye vituo vya afya na kuziuza kwenye hospitali binafsi na maduka ya dawa.

 

Hayo yameelezwa Jumanne Julai 6, 2021 na mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera katika mkutano wake na waandishi wa habari baada kupokea taarifa ya ripoti ya upotevu wa fedha kutoka kwa naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel.

 

Amesema mbali na wanachama hao kushikiliwa na polisi, pia vituo saba vya afya vimebainika kufanyika wizi wa dawa za Sh1.6 bilioni na kwamba uongozi wa mkoa huo kwa kushirikiana na wizara ya afya wametoa muda wahusika kurejesha fedha hizo.

 

“Ripoti inaeleza wizi umetokana na utoaji wa dawa kwa wanachama waliokuwa wakienda kupata huduma na kupewa dawa kwa wingi na kisha kwenda kuuza.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top