} });
 

Na, Nicholaus Lyankando, Geita

Wananchi katika kijiji cha Mgelele kata ya Isebya willayani Mbogwe wameshangazwa na kijiji chao kukosa hata nguzo za umeme hali inayowafanya wakose matumaini ya kupata huduma hiyo mbali na ahadi zinazotolewa na serikali

Wakizungumza na Divine FM baadhi ya wananchi katika kijiji hicho wamesema ni kwa muda mrefu sasa wamesha ahidiwa kuwekewa umeme lakini mpaka sasa muda walioahidiwa umeme umepita na hawaoni mikakati yoyote ya serikali kuwaletea huduma hiyo. 

Kwa upande wake diwani wa kata ya Isebya Mh. Deliton Makiao amesema, moja ya vijiji ambavyo havina umeme katika kata hiyo mojawapo ni kijiji cha Mgelele lakini akawatoa wasiwasi wananchi wawe na subira watakuja kuwekewa nguzo ikifatiwa na umeme kuwashwa. 

Hata hivyo msimamizi wa miradi ya shirika la ugavi wa umeme tanzania TANESCO wilayani Mbogwe John Ladson amesema sio kweli kwamba vijiji ambavyo havina umeme vimesahaulika kwani mpaka sasa kuna idadi ya vijiji 32 ambavyo havina umeme huku akidai awamu inayofata wananchi watarajie kufikishiwa umeme.

Wilaya ya mbogwe inajumla ya kata 17 na vijiji 84 ambapo vijiji 52 tayari vimefikiwa na huduma ya umeme. 

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top