} });
 


Kamanda wa Polisi Mkoa Mara, Longinus Tibishibwamu amewataka askari wa Dawati la Jinsia Wilaya ya Serengeti kufuatilia matukio ya ukatilli unaofanywa na wanawake dhidi ya wanaume na wazee.

Katika kikao na askari polisi Wilaya ya Serengeti, vikundi vya ulinzi shirikishi na michezo eneo la Mugumu amesema kuibuka kwa matukio ya ukatili dhidi ya makundi hayo kunatakiwa kuangaliwa zaidi.

"Msijielekeze kwa wanawake na watoto tu lakini sasa inaonekana akina baba na wazee wanafanyiwa ukatili na wake zao na wengi wao hawasemi," amesema.

Milton Peter Mkazi wa Mugumu amesema vitendo hivyo kwa sasa vinazidi kushamiri wilayani hapo na kuomba suala hilo litizamwe kwa undani kwa kuwa wengi wao wanaona aibu kutoa taarifa.

Kuhusu suala la ulinzi na usalama  amesema,"OCD Methew Mgema ameanzisha mkakati wa kuwatumia vijana kimichezo na ndani yake wanaunda timu za michezo, naomba kamanda nawe uongeze nguvu kwa kuwa matunda ni mazuri maana inatuleta raia na askari kuwa pamoja," amesema.

Hata hivyo baadhi ya vijana wameomba kuwekwe utaratibu mzuri wa namna ya kuendesha ulinzi ili kuepuka migogoro ikiwemo kuweka utaratibu wa muda wa kufungua na kufunga baa.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top