Watu
watatu wamefariki dunia baada ya kutokea mapigano ya wakulima na wafungaji
katika Kijiji cha Nanjilinji wilayani Kilwa.
Tukio hilo limetoka juzi majira ya saa saba mchana baada ya mkulima Chande
Magoma kumkuta mfugaji shambani kwake akilisha ngo'mbe mahindi yake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Mtatiro Kitinkwi amethibitisha kutoa Kwa tukio
hilo.
“Nikweli tuna tukio Kijiji cha Nanjilinji wilayani Kilwa watu wawili,
mkulima na mfugaji walipigana wakajeruliana hadi kupelekea vifo vyao wote
wawili.”
“Leo (jana) asubuhi kundi la wanakijiji wakalipiza kisasi kwa kumuua kijana
mmoja ambaye waliamini anatoka kwenye jamii ya wafugaji, tuna washikilia
watuhumia zaidi ya hamsini kuhusiana na matukio hayo, hata hivyo
kuna utulivu, baada ya viongozi ngazi ya mkoa na wilaya kufanya mkutano na
wananchi,” alisema Kitinkwi.
Post a Comment