} });
 


STRAIKA wa Yanga, Juma Mahadhi, amerejea kikosini na atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaoshiriki michuano ya Kombe la Kagame inayoanza keshokutwa Jumapili kwenye viwanja vya Mkapa na Azam Complex jijini Dar es Salaam.


Yanga imemrejesha Mahadhi aliyetolewa kwa mkopo katika usajili wa dirisha dogo msimu uliopita huko Ihefu FC Akizungumza, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassani Bumbuli alisema kuwa Mahadhi alikuwa kwa mkopo Ihefu, hivyo anarejea katika timu yake baada ya muda wa mkopo kumalizika.

“Mahadhi amerejea rasmi katika klabu yake aliyokuwa anaichezea akitokea Ihefu tulipompeleka kwa mkopo wa miezi sita pekee.“Hivyo Mahadhi ataungana na wachezaji wengine watakaokuwepo kwenye kikosi chetu kitakachoshiriki michuano ya Kagame,” alisema Bumbuli.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top