} });
 

 

Kikosi cha Young Africans kimewasili jijini Dar es salaam leo Jumatatu (Julai 26) Mchana kikitokea mkoani Kigoma kilipokua na shughuli ya kusaka ubingwa wa Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi ya Simba SC.

Mchezo huo wa Fainali Kombe la Shirikisho ulichezwa jana Jumapili (Julai 25) Uwanja wa Lake Tanganyika, na kushuhudia Simba SC wakiibuka mabingwa mara mbili mfululizo kwa ushindi wa bao 1-0.

Young Africans waliwasili kinyonge uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, huku Mashabiki na wanachama wachache wakijitokeza kuwapokea.

Bao la ushindi kwa Simba SC lilifungwa na kiungo kutoka nchini Uganda, Thadeo Lwanga dakika ya 80 kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na kiungo wa kimataifa kutoka Msumbiji, Jose Luis Miquissone.


soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top