} });
 

 

Rais wa zamani wa Afrika kusini Jacob Zuma amepewa ruhusa ya kushirikia maziko ya mdogo wake Michael anayetarajiwa kuzikwa leo mchana.

“Kwa kuwa ni mfungwa wa kifungo cha muda mfupi, mwenye hatari ndogo ya kutoroka, ombi la Zuma la kuomba ruhusa ya msiba limekubaliwa” amesema Msemaji wa idara ya kurekebisha tabia Singabakho Nxumalo mapema hii leo.

Kwa mujibu wa Nxumalo,  Zuma hatolazimika kuvaa sare za wafungwa atakapokuwa msibani.

Jacob Zuma anatumikia kifungo cha miezi 15 gerezani baada ya kukaidi amri ya kuhudhuria mahakamani kwenye kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na rushwa inayomkabili.

Wafuasi wa Zuma walifanya maandamano na vurugu ikiwemo uporaji na uchomaji moto mali mbalimbali kwa wiki mbili kupinga hukumu ya kifungo cha miezi 15 alichohukumiwa Zuma.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top