} });
 

 

Mkazi wa mtaa wa Kiongozi Mjini Babati mkoani Manyara, Lucas Mangu (46) amefariki dunia kwa kujinyonga mara baada ya kumuua mke wake Anna Kisino (41) kwa kumpiga kutokana na wivu wa kimapenzi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Marrison Mwakyoma akizungumza jana Agosti 23, 2021 amesema tukio hilo limetokea juzi usiku.

Kamanda Mwakyoma amesema Mangu alimuua mkewe kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili hadi kumuua baada ya kumfungia ndani kutokana na wivu wa kimapenzi.

Amesema Mangu alikuwa amesafiri kwenda Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro kwa ajili ya shughuli za kilimo na alirudi Babati siku hiyo na kufanya mauaji hayo ya mkewe na kujiua.
 
“Siku hiyo baada ya kurudi nyumbani ghafla bila taarifa alimkosa nyumbani mke wake ambaye alitoka kidogo na aliporudi akamuuliza alikuwa wapi na kuanza kumpiga,” amesema Kamanda Mwakyoma.

Amesema watu walijaribu kumwambia aache kumpiga mkewe baada ya kusikia yowe ila kwa kuwa alifunga mlango akimpiga aliwaambia wamuache ampige kwani ni mkewe.

“Alimpiga hadi kumuua akajaribu kumwamsha ikashindikana akadhani ni utani alipobaini amefanya mauaji akachukua mgorori akajiua kwa kujinyonga,” amesema Kamanda Mwakyoma.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top