} });
 

 

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema kuwa watu ambao hawataki kupewa chanjo ya Covid-19 waheshimiwe kwa kuwa chanjo hiyo ni suala la hiari. 

Akizungumza wakati wa ibada Jumapili Agosti Mosi, 2021, Askofu Gwajima alitumia ibada hiyo kusisitiza msimamo wake huku akisema suala la chanjo ni hiari kama ilivyopendekezwa na kamati ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema “Sizuii mtu asichanjwe, nasema wale ambao wanapenda kuchanjwa chanjweni ila mimi watu wangu nawaambia hapana tumeshavuka na wale wanaokataa kuchanjwa msimtukane Rais wangu” amesema na kuongeza

“Msimamo wa Rais aliouchukua ni msimamo ambao Rais yeyote duniani lazima auchukue” amesema Askofu Gwajima ambaye pia ni mbunge wa Kawe.

Amesema kutokana na suala la chanjo kuwa la hiari hivyo anayetaka kuchanjwa afanye hivyo huku akisema amewashauri familia yake kutokuchanjwa.

“Kila mtu anayependa kuchanja atachanjwa na baadhi watachanjwa na wale wasiotaka kuchanjwa waheshimiwe kwa sababu kamati imependekeza hivyo hata hapa ukijisikia kwenda kuchwanjwa kachanjwe sikuzuii ila mimi na familia yangu nimewashauri wanafamilia hapana” amesema Askofu Gwajima.

Pia, Askofu Gwajima amewaonya watu anodai wanaotumia msimamo wake kutaka kumgombanisha na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kile kinachodaiwa anapinga utoaji wa chanjo.

Amesema yeye kama mchungaji lazima aliongoze kundi lake kwenye njia sahihi na njia hiyo ni kutochanja na wasitokee watu wa kulazimisha kuchanja.

Askofu Gwajima alisisitiza kuwa hapingani na uamuzi wa Rais Samia wa kuleta chanjo nchini ila ameamua kufuata maelekezo ya kamati ambayo yanaeleza kuwa wananchi wataamua kuchanjwa kwa hiari.

Hii ni mara ya pili kwa kiongozi huyo wa dini kutamka hadharani kwamba hatochanjwa chanjo hiyo ya hiari na kuwataka waumini wake kutumia hiari kutochwanjwa.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top