} });
 

 

Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufunuo lililopo Kimara Bonyokwa, Mchungaji Paul Bendera amewashukia baadhi ya viongozi wa dini wanaowashawishi waumini wao na wananchi kuwa wasichanje chanjo ya virusi vya corona kwa madai ya kwamba itaharibu mifumo yao ya miili.

 

Askofu Bendera amesema hayo jana Jupamili, Agosti 1, 2021 wakati akihubiri katika ibada kanisani hapo na kuongeza kuwa endapo chanjo hiyo ingekuwa na madhara basi Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan asingekubali kujiingiza kwenye matatizo kupikea chanjo, kuchoma yeye mwenyewe na kuchanja walinzi wake, watumishi wa afya na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

 

Bendera amesema kuwa iwapo Wazungu wangekuwa na nia ya kutumaliza kupitia chanjo kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakipotosha basi wangekuwa wameshafanya zamani lakini chanjo hii imethibitishwa na vyombo vya masuala ya afya duniani kuwa ni salama kwa binadamu hivyo amewataka waumini wake kwa hiari yao kuchanja ili kuondokana na uwezekano wa kuambukizwa gonjwa hilo hatari na kupoteza maisha yao.

 

Aidha, Bendera amesema amesema yeye tayari ameshachanjwa baada ya kujiridhisha ni salama hivyo wananchi wasiwasikilize wapotoshaji kwani chanjo nyingi zipo tangu zamani na hakuna ambaye amekuwa nazo shaka ilihali zinatoka huko huko kwa wazungu.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top