} });
 

 

Klabu za AFC Leopards na Gor Mahia zimekatwa alama tatu kila mmoja na kutozwa faini ya Kshs milioni 10 baada ya kugomea mchezo wao wa Ligi Kuu ya Kenya ambao ulipangwa kufanyika juzi Jumamosi (Julai 31).

Timu hizo mbili, kupitia mawasiliano ya pamoja yaliyosainiwa na Dan Shikanda, kwa niaba ya Ingwe, na Ambrose Rachier ambaye aliiwakilisha K’Ogalo walidai wanalidai pesa Shirikisho la soka huko Kenya “FKF” za udhamini na zawadi ya Kombe la FKF kama mshindi wa kwanza na wa pili jumla ya Ksh 3 milioni, na kweli hawakucheza mchezo huo baada muda waliotaka pesa ili wacheze kutotimizwa.

Kamati ya Ligi na Mashindano imesema, barua zilitumwa kwa vilabu vyote viwili, huku vikitakiwa kulipa pesa zao kabla ya Agosti 5,.

Gor wametizwa faini ya Ksh 4 milioni na Leopards imepigwa faini ya Ksh 6 milioni na wote kwa pamoja wameondolewa alama tatu za ligi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top