} });
 


Kocha wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) Kim Poulsen amewasamehe na kukubali kuwapokea wachezaji wa Simba SC Shomar Kapombe na Erasto Nyoni.

Jana Jumanne (Agosti 24) usiku, ilielezwa kuwa Kocha Poulsen alishindwa kuwapokea wachezaji hao kambini, kwa madai wamechelewa kuripoti, licha ya kuwasili Dar es salaam mapema wakitokea nchini Morocco.

Taarifa za kukataliwa kambini kwa wachezaji hao ziliongeza kuwa muda alioweka kocha huyo kwa wachezaji hao ulikuwa ni saa kumi na moja jioni lakini wachezaji hao walichelewa kuingia kambini na kufika usiku wa saa tano.

Hata hivyo imeelezwa kuwa Kocha Poulsen alitumia muda wake kuwasikiliza na aliamua kuwasamehe na kuwapokea.

Taifa Stars imeingia kambini kujiandaa na mchezo wao wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya DR Congo na Madagascar.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top