} });
 

 

Katika hali ya Mshtuko Mjumbe wa kamati ya utendaji wa Young Africans Athuman Kihamia ametangaza kujiuzulu nafasi yake ndani ya klabu hiyo.

Maamuzi ya Kihamia yamekuja saa chache baada ya Uongozi wa Young Africans kumtangaza aliyekua Msemaji wa Simba SC Haji Manara kuwa mwanafamilia wa klabu hiyo.

Kihamia ametangaza kujiuzulu pasina kutoa sababu maalum, zaidi ya kuwaaga wajumbe wenzake na wanachama wa Young Africans.

“Wajumbe wenzangu, Habarini za jioni, Nichukue nafasi hii kuwajulisha rasmi kuwa nimejiuzulu nafasi yangu ya ujumbe wa kamati ya Utendaji, Yanga SC kuanzia Leo, Tarehe 24, Agosti 2021 usiku huu Asanteni.” Ni maneno ya Kihamia.

Mpaka sasa Uongozi wa Young Africans haujatoa taarifa zozote kuhusu kujiuzulu kwa mjumbe huyo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top