} });
 

Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge

Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge, amewataka watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Kagera kufanya kazi kwa weledi na kuepuka matumizi ya lugha zisizofaa kwa wagonjwa wanaofika hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya hospitali ya rufaa ya mkoa, Meja Jenerali Mbuge, amesema kuwa yapo malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wakilalamikia huduma zisizoridhisha na matumizi ya lugha zisizofaa kwa wagonjwa, na kuitaka bodi mpya kuhakikisha malalamiko hayo hayasikiki tena 

"Hali inakatisha tamaa kwa wagonjwa wanaokuja kupata huduma utakuta mgonjwa amekuja anaumwa anataka apate tiba lakini anapopewa huduma isiyoridhisha basi ule ugonjwa unaongezeka mara mbili, ni mategemo yangu mwenyekiti wa bodi na wajumbe wote tuone tunatoa huduma nzuri kwa wananchi wetu," amesema RC Mbuge.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Pius Ngeze ameahidi kufanyia kazi maagizo hayo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa huku akiwataka watumishi wa hospitali hiyo kuheshimu wagonjwa, na kwamba hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa watakaokiuka agizo hilo ili kukomesha vitendo hivyo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top