
Mashahidi
24 na vielelezo 19, wanatarajia kutoa ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi
inayomkabili, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Freeman Mbowe na wenzake watatu.
Miongoni mwa mashahidi hao, yupo aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Boaz.
Hayo yameelezwa
leo, Agosti 23, 2021 na upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali
Mwandamizi, Nassoro Katuga akisaidiana na Ester Martin, wakati wakiwasomea
maelezo ya mashaidi na vielelezo (Commital Proceedings) washtakiwa hao, mbele
ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment