} });
 

 

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimepokea kwa masikitiko barua ya kujiuzulu kwa Mbunge Mteule wa CCM Jimbo la Konde Sheha Mpeka Faki leo August 02, 2021.

“Katika barua ya Sheha ameeleza kwamba amefikia uamuzi huo kutokana na changamoto za kifamilia jambo ambalo Chama hakina uwezo wa kumzuia hasa ikizingatiwa kwamba ni haki yake ya msingi kama ilivyo kwa haki ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ndani ya CCM” - Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Sheha Faki amejiuzulu siku chache tu baada ya kutangazwa Mbunge mpya na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika Jumapili 18 Julai 2021.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top