} });
 


Mfanyakazi wa Kampuni ya MMJ Steel Ltd, Adamu Thabit (28) na Mkurugenzi wa Bongo News YouTube, Heri Said (29), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu, likiwemo la kuchapisha maudhui ya uongo mtandaoni dhidi ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga akisaidiana na Faraja Ngukah, mbele ye Hakimu Mkazi Mwandamizi, Evodia Kyaruzi.

Akiwasomea mashtaka yao, Katuga alidai katika shtaka la kwanza, Juni 20, 2021 katika maeneo tofauti ya mkoa wa Dar es Salaam, walichapisha picha na maelezo katika mfumo wa ujumbe mfupi wa maandishi uliosomeka “Ghafla Waziri Mkuu atumbuliwa, avujisha video picha zake za ngono” huku wakijua ujumbe huo ulikuwa ni wa uongo na ulikuwa na lengo la kupotosha umma.

Shtaka la pili ni kuendesha chaneli ya Youtube bila kuwa na leseni, kosa ambalo wanadaiwa kutenda kati ya Januari 2, 2018 na Julai 2, 2021 katika mkoa na jiji la Dar es Salaam.

Kupitia chaneli hiyo yenye jina la Bongo News, walirusha maudhui yenye kichwa cha habari “Ghafla Waziri Mkuu atumbuliwa, avujisha video picha zake za ngono” bila kuwa leseni kutoka TCRA.

Shtaka la tatu ni kuchapisha maudhui yasiyoruhusiwa, shtaka lililosomwa na wakili Ngukah, kuwa Juni 20, 2021 katika jiji hilo kwa makusudi walichapisha maudhui yasiyoruhusiwa kupitia mtandano wa You Tube wa Bongo News, maudhui ambayo yalionyesha picha za ngono zilizomhusisha waziri mkuu.

Washtakiwa walikana kutenda makosa hayo na upande wa mashtaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Pia upande wa mashtaka ulipinga wasipate dhamana kwa sababu tuhuma zinazowakabili zinamhusu kiongozi mkubwa wa nchi, hivyo waendelee kukaa ndani kwa ajili ya usalama wao hadi pale hali itakapotulia.

“Lakini kama mahakama ikiona wana haja ya kuwapa dhamana, itumie sheria hiyohiyo na washtakiwa wasitoke nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kuwa na kibali na wawasilishwe hati zao za kusafiria mahakamani hapa,” alidai Katuga.

Washtakiwa walipingana na hoja ya Jamhuri, wakidia hata Julai 2, 2021 walipopelekwa polisi walipata dhamana na hakukuwa na tishio lolote la kiusalama mtaani.

Kutokana na hali hiyo, Hakimu Kyaruzi alisema atatoa uamuzi leo kama washtakiwa watapata dhamana. Washtakiwa walirudishwa rumande hadi leo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top