Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amewataka wakazi wa Dodoma kuchukua hatua za
tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona kwa sababu hali si nzuri mkoani humo.
Ameyasema
hayo leo Jumanne Agosti 3, 2021 wakati akizungumza na askari wa usalama wa
barabarani na viongozi wa masoko wa mkoa wa Dodoma.
Amewataka
askari hao, viongozi wa masoko na wafanyabiashara kuhakikisha wanachukua hatua
za kujikinga katika maeneo yao kwa kuvaa barakoa na kunawa maji tiririka na
sabuni au kutumia vitakasa mikono.
Pia
amewataka askari wa usalama wa barabarani kuhakikisha watu wote wanakaa kwenye
viti (level seat) kwenye daladala na bajaji na kwenye bodaboda kuhakikisha
hawabebi abiria zaidi ya mmoja.
Mkuu
wa Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, Boniface Mbao amesema watakapotoka katika
kikao hicho wataenda kutekeleza maagizo hayo kwa kutoa elimu na ikibidi kwa
ukali, ili kuhakikisha abiria wanakaa katika viti kwenye mabasi ya abiria.
Amesema hakuna gari litakalopita kwenye mkoa huu likiwa limejaza zaidi ya abiria waliokaa kwenye viti.
Post a Comment