} });
 


Tangu ameondoka Kocha Lucy Eymael katika kikosi cha Young Africans, Beki Said Juma Makapu amekuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha klabu hiyo, licha ya kwamba akipewa nafasi hufunika sana.

Makapu kiasili ni Kiungo mkabaji na nafasi hiyo amekuwa akicheza Mukoko Tonombe na muda mwingine hutumika kama Beki wa kati ambapo hutumika Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Lamine Moro, ambaye ameshaagwa Young Africans.

Kocha wa Mtibwa Sugar, Mohammed Badru anaamini mchezaji huyo kiraka anaweza akamfaa kwenye mipango yake ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, na tayari amewaachia viongozi wa kkabu hiyo kufanikisha mpango wa kumsajili.

Mbali na Makapu Badru amependekeza usajili wa wachezaji wapya wasiopungua watano, ambao anaamini watairudisha kwenye hadhi Mtibwa Sugar.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top