} });
 


Mume wa msanii Shilole, Rommy 3D ameonyesha kutofurahishwa na wanaoponda muonekano wa unene wa mke wake huyo, na kuvunja ukimya kwa wote wanaotaka apungue kuwa hawaitakii mema ndoa yao.

Maoni yamekuwa mengi baada ya performance yake siku ya jana kwenye kilele cha Wiki ya Wananchi baada ya kutumbuiza na mashabiki kupata nafasi ya kuuona muonekano wa mwili wake huku wengi wakishauri apungue.

“Woote wanaotaka mke wangu apungue hawaitakii mema ndoa yetu (ni wachawi) kwasababu kwenye historia yangu sijawahi kupenda dem kimbaumbau, napenda mabonge haswaaaa (wanaonijua wanajua)”.

Rommy 3D aliendelea kumtetea mke wake huyo kupitia instagram kwa kuandika “Mke wangu Shilole wasikudanganye endelea kunenepa mama, Nakupenda!!!”

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top