} });
 

 

Mbunge wa jimbo la Muheza Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA, amepata ajali ya gari eneo la Mkambalani mkoani Morogoro jana Agosti 31, 2021 usiku.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Fortunatus Muslim na kueleza kuwa mbunge huyo yupo salama.

Kwa upande wake Mwana FA alipopata nafasi ya kuongea na waandishi wa habari alieleza kuwa kabla ya ajali waliona gari mbele yao inataka kupita gari (Overtake) na ilikuwa mwendokasi sana hivyo hawakuweza kuikwepa ndio ikawaparamia.

Picha kutoka eneo la ajali

Aidha amesema kiafya yeye na mwenzake aliyekuwa naye kwenye gari ni wazima ila alikuwa anasikia maumivu kidogo kifuani mwake.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top