} });
 

 

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo leo Agosti 23, 2021 amezungumza kuhusu mfumo mpya wa ulipaji wa kodi ya Majengo.

“Naomba niweke wazi Wananchi wasiwe na taharuki nyumba za Vijijini haziko katika mpango wa kutozwa kodi ya majengo vilevile nyumba zilizojengwa kwa vifaa ambavyo sio vya kudumu kama zile udongo zilizoezekwa kwa nyasi hazihusiki na kodi ya majengo” - Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi TRA

“Kodi ya majengo ni kodi ambayo inatozwa kutokana na maendelezo juu ya ardhi, mara nyingi Watu wanaichanganya na kodi ya ardhi, hii kodi ya ardhi inalipwa kule Wizara ya ardhi kodi ya pango la ardhi ni ardhi ambayo haina chochote au ina jengo juu yake, kodi ya jengo ni yale maendelezo juu ya ardhi ndio inayolipwa kwa sasa” - Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi TRA

“Na kodi hii mwanzoni ilikuwa ikikusanywa na wenzetu wa Local Government na baadae ikahamishiwa TRA na wakati tunaanza kuikusanya utaratibu ulikuwa tofauti kidogo ilikuwa jengo linathaminishwa alafu inatozwa kwa asilimia fulani ya hiyo thamani ya jengo”- Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi TRA

“Kiukweli utaratibu huu ulikuwa na usumbufu sana utakuta nyumba zilizothaminishwa zinakuwa ni chache ukilinganisha ambazo hazijathaminishwa, utakuta mtaa mwingine nyumba yake imethaminishwa analipa asilimia na mwingine nyumba yake haijathaminishwa analipa Tsh. Elfu 10 “ - Mkurugenzi wa Huduma na Elimu Kwa Mlipa kodi Richard Kayombo

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top