} });
 

 

Meneja wa Paris Saint-Germain, Mauricio Pochettino ameanza msimu wa 2021/22 kwa kichapo kutoka kwa Mabingwa watetezi wa Ligue 1, Lille walipopata ushindi wa bai 1-0 kwenye mchezo wa French Super Cup.

Goli la kipindi cha kwanza kutoka kwa Xeka lilitosha kuwavua Ubingwa wa French Super Cup PSG baada ya kuubeba mara nane zilizopita, na Lille kunyakua kwa mara ya kwanza katika historia baada ya kupoteza 1955 na 2011.

Pochettino hakuwa na washambuliaji nyota kama Kylian Mbappe na Neymar lakini bado aliweza kuweka safu ya ulinzi yenye uzoefu ikiwa na Achraf Hakimi na Presnel Kimpembe, pia Ander Herrera na Mauro Icardi walikuwa miongoni mwa wachezaji walioanza.

Lille inakua klabu ya saba kubeba ubingwa wa French Super Cup baada ya PSG (10), Lyon (7), Bordeaux, Marseille, Monaco na Nantes (wote mara mbili kila mmoja).

Pia ni mara ya kwanza kwa klabu nyingine nje ya PSG kushinda kombe hilo tangu mwaka 2012 (Lyon v Montpellier).

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top