} });
 

 

Rais wa Znz na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Hussein Ali Mwinyi ameivunja Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) kuanzia tarehe 18 August 2021 na kumteua Ramadhan Mwalim Khamis kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo ambapo uteuzi huo umeanza Aug. 18 2021.

Rais Dr. Mwinyi pia amemteua Balozi Amina Salum Ali kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Takwimu Zanzibar kuanzia tarehe 16 August 2021, pia Rais wamefanya uteuzi wa Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Watu wenye ulemavu kama ifuatavyo… Bibi Salma Haji Saadat ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wenye ulemavu huku Bwana Ussy Khamis Debe akiteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Watu wenye ulemavu, uteuzi huu umeanza tarehe 18 August 2021.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top