} });
 


Rais Samia Suluhu Hassan amelitaka Jeshi la Polisi Tanzania kukaa na wadau kuangalia  uwezekano wa kurekebisha sheria ya kuweka mtu mahabusu.

Akizungumza leo Jumatano Agosti 25, 2021 wakati akifungua kikao kazi cha maofisa wa polisi,   amesema itasaidia kuipunguzia Serikali mzigo wa kuhudumia maelfu ya watuhumiwa waliopo mahabusu wakati hakuna ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani

“Lakini kwa upande mwingine mwanadamu ni mwanadamu na ana uhuru wake naomba mkae  na wadau wengine muangalie uwezekano wa kurekebisha sheria ya kuweka mtu mahabusu, kwenye nchi nyingine mtu hakamatwi mpaka upelelezi umetimia,   akikamatwa anawekwa ndani wiki, siku tatu nne tayari mahakamani anahukumiwa anaendelea."

“Huwezi kukuta Serikali inabeba mzigo wa mahabusi ushahidi haujakamilika naomba muangalie hayo mambo ili tutoe huduma zinazofaa kwa watu wetu, " amesema Samia

Kiongozi mkuu huyo wa nchi amesema hadi Agosti 22, 2021 takwimu zinaonyesha kuna mahabusu 15, 194 idadi inayokaribiana na wafungwa ambao wako 16, 542.

“Sasa mahabusu hawa kuna waliokaa wiki, miaka miwili, miaka mitatu, mwaka, muda mbalimbali na kila anayeguswa upelelezi haujakamilika, sasa nitoe wito mara mbili, mara moja kwa zile kesi ambazo mna hakika upelezi hautokamilika hao watu watolewe wakafaidi uhuru wao wakiwa nje."

"Kama kesi haina muelekeo na hili nalisema sijui  mara ya pili sijui ya tatu basi hao watu watolewe, lakini kwa zile kesi ambazo mnahakika upelelelezi utatimia basi uhalakishwe kama mlivyojiweka muda, " amesema.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top