} });
 


Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania imesema imeanza utekelezaji wa kukusanya kodi ya majengo kwa kutumia mfumo mpya wa ukusanyaji kupitia ununuzi wa umeme, utekelezaji utaanza rasmi August 20,2021 na unafanyika chini ya usimamizi wa TRA kwa kushirikiana na TANESCO ukihusisha mita za aina zote za Umeme.

Kwa njia hii mpya ya ukusanyaji wa kodi kila mnunuzi wa umeme atakatwa Tsh.1000 kwa Mwezi kwa nyumba ya kawaida na Tsh. 5000 kwa Mwezi kwa sakafu ya ghorofa, kwa wanaotumia mita za ankara watalipia kodi hii kwa pamoja katika ankara ya mwezi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top