Msanii Amber Rutty amefunguka tukio la kupigwa na mumewe Davil kumesababisha kutokwa na damu nyingi hali iliyofanya kumpoteza mtoto tumboni kwa sababu alikuwa mjamzito.
Amber Rutty anasema sababu zilizofanya kupigwa na mumewe ni kufumwa na 'message' alizokuwa anawasiliana na msanii Enock Bella ambaye anadai alikuwa anamtongoza.
Pia msanii huyo ameongeza kusema hiyo ni mara ya pili kupigwa na mumewe, kwa sasa amefikisha jambo hilo katika vyombo vya sheria na anadai talaka ili waweze kuachana.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment