} });
 

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makala ametoa siku ya jumapili wiki hii kua siku ya chanjo kimkoa ambayo itatolewa katika uwanja wa Taifa kwa watu wote bila kuangalia umri.

RC Makalla amesema Jumapili Agosti 22, 2021 kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi jioni wakazi wa Dar es Salaam wajitokeze kupata chanjo ya Uviko-19 na endapo mda wa saa kumi watakua bado hawajamalizika mda utaongezwa mpaka wote wamalizike.

RC Makalla ameeleza hayo leo Alhamisi Agosti 19, 2021 wakati akizungumza na watendaji na wafanyakazi wa manispaa ya Temeke katika kikao kazi cha halmashauri hiyo.

Amesema mchakato utawahusu wananchi wote wenye umri wa kuanzia miaka18 ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakikosa muda wa kwenda kupata huduma hiyo katika vituo vilivyoanishwa mkoani Dar es Salaam.

Akieleza sababu ya kuweka siku ya jumapili Watu wachanjwe kwa hiari yao Makalla amesema ni baada ya kupokea malalamiko katika mitandao ya kijamii na simu kuwa Wananchi wakieleza kukosa huduma hiyo kutokana na foleni kubwa na majukumu mengine ya kazi

Katika hatua nyingine amewaagiza Wakuu wa wilaya zote za Dar es salaam kuweka siku moja ambayo itawaruhusu Watumishi wote na Wananchi kupata chanjo kwa hiari yao kuwezesha Watu wengi kupata chanjo.

"Kilio cha chanjo hasa wanaofanya kazi kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa na kukosa muda kimesikika, sasa chanjo itatolewaa Jumapili katika eneo la wazi kuanzia saa 2 asubuhi. Tutakuwa na wahudumu 100 kwa ajili ya shughuli hii," amesema RC Makalla

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top