} });
 


Na Faustine Gimu Galafoni - Dodoma

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini, Jabir Shekimweri amepiga marufuku kitendo cha wapigadebe  na bodaboda  kituo kikuu cha mabasi Dodoma kulazimisha abiria  wanaokwenda mjini kuwashushia kituoni hapo hata kama  hawana uhitaji wa kushukia pale.

Marufuku hiyo ameitoa alipofanya ziara kituoni hapo baada ya kupokea malalamiko ya baadhi ya abiria kuwa wamekuwa wanalazimishwa na wapiga debe kushukia kituo kikuu cha mabasi Dodoma  wapande bodaboda licha ya kuwepo mabasi  ya mikoani  yanayopitiliza mpaka mjini Dodoma.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya ametembelea eneo lenye ukubwa wa ekari nane lililotengwa kwa ajili ya wajasiliamali  lililopo katikati ya Kituo ya kikuu cha mabasi na soko kuu la Ndugai na kutoa ushauri namna nzuri zaidi ya upanuzi wa maeneo ya wajasiriamali  huku mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumzia manufaa yatakayopatikana kutokana na eneo hilo .

Awali akitolea maelezo juu ya eneo hilo la wajasiriamali ,afisa maendeleo jiji la Dodoma Hidaya Mizega amesema kutakuwa na kiwanda cha kusindika maziwa na ngozi huku mstahiki meya Prof.Davis Mwamfupe akisema hatua hiyo ni namna bora ya baraza la madiwani kutumia asilimia 10 ya mkopo ambapo  afisa wa jeshi la zimamoto na uokoaji   Dodoma  Inspekta Deogratius Inano akisema  ni muhimu jeshi hilo kushikikishwa .

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top