} });
 


Watoto wawili wa familia moja wakazi wa Tarakea wilayani Rombo wamefariki baada ya nyumba yao waliyokuwa wakiishi kuungua kwa moto.

Akitoa taarifa hiyo leo Ijumaa Agosti 20, 2021 Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Hamis Maiga ameeleza tukio hilo limetokea jana usiku uliosababishwa na mshumaa.

Hamisi amesema watoto ambaye mmoja ana miaka sita, na mwingine ana mwaka mmoja

"Mwanamke mmoja mwenye watoto wawili aliwasha mshumaa baada ya luku yao kwisha, baada ya kuwasha mshumaa akawa ametoka nje kidogo.

“Mshumaa alikuwa ameweka kwenye meza ya plastiki ndipo mshumaa ulipodondokea kwenye meza na kushika kwenye mabanzi ambayo yalishika moto na nyumba yote yenye vyumba 10 kuteketea," amesema Maiga.

Maiga amesema kwa sasa Kamati ya Ulinzi ya wilaya hiyo inaelekea kwenye eneo la tukio.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top