} });
 

 

Watu 10 wamefariki dunia na nane kujeruhiwa baada ya gari la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kugongana Uso kwa Uso na gari la mizigo katika Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Ilalwe kata ya Bukombe wilayani Bukombe na kuhusisha gari la jeshi lililobeba ndugu waliotoka kwenye msiba wilaya ya Kahama likigongana na gari ya mizigo.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Said Nkumba amesema Majeruhi Sita walihamishiwa katika hospitali ya Ushirombo na wawili wapo kituo cha afya Masumbwe na miongoni mwa marehemu yupo Mwanajeshi mmoja.

Miili ya waliopoteza maisha imehifadhiwa hospitali ya Masumbwe na chanzo cha ajali bado hakijafahamika na Jeshi la Polisi linandelea na uchunguzi kwenye eneo la tukio.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top