} });
 


Kurejea madarakani kwa Taliban nchini Afghanistan, kumezilazimu nchi za Magharibi kuondoa haraka raia wao na Waafghan walio katika hatari kutoka uwanja wa ndege wa Kabul, kwa kuhofia ulipizaji kisasi kutoka kundi hilo.

Operesheni hii kubwa, ilioanza Agosti 14, imewezesha kuondoa watu zaidi ya 123,000, kulingana na takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na makao makuu ya jeshi la Marekani, Pentagon.

"Ikiwa operesheni hii ya wanajeshi imekamilika, shughuli ya kidiplomasia kuhakikisha kwamba kuna Wamarekani na Waafghan walio katika hatari ambao wanataka kuondoa, inaendelea," amesema Jenerali Kenneth McKenzie, Kamanda mkuu wa jeshi la Marekani katika eneo hilo.

Marekani inasikitishwa na vifo 2,456 na gharama ya dola bilioni 2,313 kwa miaka 20, kulingana na utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Brown. Wanatoka kwenye vita hii na picha iliyochafuliwa zaidi na kushindwa kutabiri kasi ya ushindi wa Taliban na usimamizi wao katika operesheni ya uokoaji.

Wamarekani wengi wana mashaka juu ya nia njema ya Taliban

Joe Biden ametetea uamuzi wake wa kuondoa wanajeshi wa Marekani kwa kukataa kuongeza muda wa vita hivi na kubaini kwamba lengo lao lilikuwa limekamilika baada ya kifo cha Bin Laden, aliyeuawa na vikosi maalum vya Marekani mnamo mwaka 2011 nchini Pakistan.

Hata hivyo rais Joe Biden alitoa taarifa fupi kuwashukuru wale wote waliohusika katika operesheni ya uokoaji kwa siku 17 zilizopita na kusema kuwa atalihutubia taifa baadaye leo Jumanne.

Waafghan wana wasiwasi na utawala wa Taliban

Waafghanistan wengi wanaangalia utawala wa Taliban katika maeneo ya vijijini na wanahofu kuwa hawajabadilika, lakini kwa namna fulani wamezidi kuwa wabaya.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top