} });
 


Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Iguda,  Limi Kulwa(30) amekatwa mapanga hadi kufa na mumewe aliyemtuhumu kuwa amemuua baba yake mzazi.

 

Kwa mujibu wa kamanda wa  polisi mkoani Shinyanga, George Kyando, tukio hilo limetokea jana Septemba 27, 2021 katika kijiji hicho kilichopo kata ya Iyenye halmashauri ya manispaa ya Kahama.

 

Amesema  chanzo cha tukio hilo ni imani za kishirikina ambapo mtuhumiwa alimtuhumu  mkewe kumroga na kumuua baba yake mzazi, Lusana Kulwa(60) aliyefariki dunia Julai, 2021.

 

“Alimkuta mkewe nje anapika na kumshambulia kwa panga kwa  kumkata kichwani, usoni pamoja na mikono yake miwili, baada ya kutekeleza tukio hilo mtuhumiwa alitoweka  kusikojulikana na mpaka sasa polisi tunamsaka," amesema Kyando akiongeza kuwa wanawashukilia watu sita wa familia moja kutokana na mauaji hayo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top