
Baada ya vikosi vya Jeshi la Guinea kutangaza kuipindua serikali ya nchi hiyo iliyokuwa chini
Rais Alpha Conde, Jeshi hilo limetoa amri ya kutotoka nje usiku nchini kote, hadi itakapotolewa
taarifa nyingine, na nyadhifa zote za magavana kuchukuliwa na jeshi.
Aidha, Kundi la wanajeshi waliofanya mapinduzi kupitia taarifa iliyosomwa katika televisheni ya
taifa limesema litaitisha baraza la mawaziri la serikali ya Conde na maafisa wengine wa ngazi
juu saa tano asubuhi majira ya huko.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment