} });
 


Bunge la Jamhuri ya Muungano limepitisha muswada wa sheria unaotamka kuwa kukutwa na bangi, mirungi sasa ni kosa la jinai.

 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardius Kilangi aliwasilisha muswada huo bungeni jana Jumanne Septemba 7, 2021 ambapo muswada umeongeza uzito wa bangi na mirungi kwenye makosa yanayosikilizwa katika Mahakama Kuu na mahakama za wilaya.

 

Profesa Kilangi amesema awali sheria haikutamka kama ni kosa la jinai ingawa ilizuia kitendo hicho bila kutamka jinai.

 

Mirungi na bangi ni miongoni mwa dawa za kulevya ambazo Serikali imekuwa ikipambana kukomesha vitendo hivyo kama ilivyo kwa dawa zingine.

 

"Lengo la marekebisho haya ni kupunguza mrundikano wa kesi mahakama za wilaya zinazosubiri kupelekwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikilizwa," amesema Kilangi.

 

Amesema mbali na marekebisho ya vifungu vya 15 na 15A katika kuongeza uzito huo, kifungu cha 17 kinarekebishwa ili kufanya kuwa kosa la jinai kitendo cha kukutwa na au kutumia kiwango kidogo cha dawa za kulevya.

 

Amesema kwa sasa, sheria inazuia kitendo hicho bila kutamka kuwa ni kosa la jinai jambo lililoonekana kuwa na upungufu wa kisheria wakati wa kutoa haki.

 

Wabunge waliotoa maoni yao kwa kukubaliana na pendekezo la Mwanasheria Mkuu hivyo wanasubiri saini ya Rais ili kuwa sheria kamili.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top