
Mwandishi wa Habari wa ITV/Radio One Mkoa wa Songwe, Gabriel Kandonga amefariki Dunia katika ajali ya gari iliyotokea leo asubuhi katika eneo la Karasha mji mdogo wa Mlowo Mkoa wa Songwe.
Ripoti zinasema Kandonga alikuwa kwenye gari binafsi na mwenzake Aika Sanga, Mwandishi wa Clouds TV ambae amejeruhiwa na anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Songwe.
Tunatoa pole kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Kandonga pamoja na ITV/Radio One kwa kuondokewa na Mpendwa wao.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment